Dhibiti

Una uwezo wa kudhibiti faragha yako.

Tunatumia data ili kukupa huduma bora kadiri tuwezavyo, lakini ni wewe utakayeamua aina ya data tutakayokusanya na kutumia. Tumetengeneza kipengele cha Akaunti Yangu ili kukuwezesha ufikie haraka zana rahisi utakazotumia kudhibiti faragha na usalama wako. Ni wewe utakayeamua jinsi data yako inavyoweza kuboresha huduma za Google kwa manufaa yako kwa kukagua mipangilio ifuatayo.

Nenda kwenye Akaunti Yangu

Dhibiti mipangilio yako ya faragha kwa kutumia zana ya Ukaguzi wa Faragha

Kwa dakika chache tu, unaweza kudhibiti aina ya data inayokusanywa na Google, kusasisha maelezo unayoshiriki na marafiki au hadharani, na kudhibiti aina ya matangazo ambayo ungependa Google ikuonyeshe. Unaweza kubadilisha mipangilio hii wakati wowote.

Fanya Ukaguzi wa Faragha

Linda akaunti yako kwa kutumia zana ya Ukaguzi wa Usalama

Jambo la kwanza unaloweza kufanya ili kulinda Akaunti yako ya Google ni kufanya Ukaguzi wa Usalama. Tulibuni zana hii ili kukusaidia kuthibitisha kuwa maelezo yako ya kurejesha akaunti yamesasishwa, na kwamba tovuti, programu na vifaa vilivyounganishwa na akaunti yako ndivyo unavyotumia na kuamini. Kama unashuku kitu chochote, unaweza kubadilisha mipangilio yako au nenosiri mara moja. Ukaguzi wa Usalama huchukua dakika chache tu, na unaweza kuufanya mara nyingi utakavyo.

Fanya Ukaguzi wa Usalama

Bainisha aina ya data itakayohusishwa na akaunti yako

Data tunayohifadhi kupitia akaunti yako inaweza kufanya huduma za Google zikufae zaidi, kama vile kupata chaguo bora za usafiri katika Ramani za Google na matokeo ya haraka katika huduma ya Tafuta na Google. Kwa kutumia Vidhibiti vya Shughuli, unaweza kubainisha data itakayohusishwa na akaunti yako na kusitisha ukusanyaji wa aina mahususi ya data, kama vile shughuli zako za utafutaji na kuvinjari mtandaoni, mahali unapoenda na maelezo kutoka vifaa vyako.

Nenda kwenye Vidhibiti vya Shughuli

Dhibiti matangazo kulingana na mambo unayopenda

Katika Mipangilio yako ya Matangazo, unaweza kudhibiti matangazo kulingana na mada unazopenda. Kwa mfano, kama unatumia mipangilio ya Mapendeleo ya Matangazo, ili kuambia Google kuwa unapenda muziki wa Rumba, unaweza kuona matangazo ya rekodi zitakazotolewa hivi karibuni na tamasha zilizokaribu nawe unapoingia katika akaunti ya YouTube.

Unapozima kipengele cha Mapendeleo ya Matangazo ikiwa umeingia katika akaunti, tataacha kukuonyesha matangazo yanayohusiana na mambo unayopenda kwenye huduma za Google na kwenye tovuti na programu za washirika wetu. Ikiwa umeondoka katika akaunti, kuzima Mapendeleo ya Matangazo kutaathiri huduma za Google mahali ambapo matangazo yanaonyeshwa pekee.

Nenda kwenye Mipangilio ya Matangazo

Angalia aina ya data iliyo katika akaunti yako kwenye Shughuli Zangu

Sehemu ya Shughuli Zangu ni mahali ambapo unaweza kupata mambo ambayo umetafuta, kuangalia na kutazama kwa kutumia huduma zetu. Ili uweze kukumbuka mambo uliyotafuta awali mtandaoni kwa urahisi, tunakupa zana za kutafuta kulingana na mada, tarehe na bidhaa. Unaweza kufuta kabisa shughuli mahususi au hata mada zote ambazo huhitaji katika akaunti yako.

Nenda kwenye Shughuli Zangu

Kagua maelezo ya msingi ya akaunti yako

Dhibiti aina ya maelezo ya kibinafsi unayoshiriki kwenye huduma za Google, kama vile jina, anwani ya barua pepe na nambari yako ya simu.

Kagua Maelezo Yako ya Kibinafsi

Tumia maudhui yako popote ulipo kwa kutumia zana ya Pakua Data Yako

Picha zako. Barua pepe zako. Anwani zako. Hata alamisho zako. Ni wewe unayedhibiti maudhui yaliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Hiyo ndiyo sababu iliyotufanya tukaunda Pakua Data Yako — ili uweze kunakili, kuhifadhi nakala rudufu au hata kuihamishia kwenye huduma nyingine.

Nenda kwenye Pakua Data Yako