Intaneti Salama

Tunasaidia kudumisha usalama wa kila mtu kwenye intaneti.

Tuna historia ndefu ya kuendeleza teknolojia ya usalama kwa manufaa ya watumiaji wetu na watu wengine wanaotumia mtandao. Tunapobuni teknolojia ya kuboresha usalama wa huduma zetu, tunapata fursa ya kuishiriki kwa manufaa ya kila mtu. Kadiri hatari zinapobadilika, ndivyo tunavyochukua hatua zinazofaa kuzikabili kabla ya kampuni nyingine.

Kuvinjari Salama hulinda watumiaji wengine kando na wale wa Chrome

Tulibuni teknolojia ya Kuvinjari Salama ili kulinda watumiaji wa Chrome dhidi ya programu hasidi na majaribio ya kuhadaa ili kupata maelezo ya kibinafsi, kwa kuwatahadharisha wakati wanapojaribu kutembelea tovuti hatari. Ili kufanya Intaneti iwe salama kwa manufaa ya kila mtu, tuliruhusu kampuni nyingine zitumie teknolojia hii katika vivinjari vyao, ikiwa ni pamoja na Apple Safari na Mozilla Firefox bila malipo. Kufikia sasa, teknolojia ya Kuvinjari Salama inalinda asilimia hamsini ya wanaotumia mtandao.

Tunatahadharisha pia wamiliki wa tovuti wakati tovuti zao zina hitilafu za kiusalama na kuwapa zana za kuwasaidia kusuluhisha hitilafu hizo bila malipo. Kwa kushiriki teknolojia mpya ya usalama tunapoendelea kuiboresha, tunasaidia kuimarisha usalama wa Intaneti kwa manufaa ya kila mtu.

Tunatumia HTTPS kukulinda unapotumia Intaneti

Kuunganisha kwenye huduma zetu kupitia usimbaji fiche wa HTTPS hukulinda dhidi ya washambuliaji na wavamizi wa programu mtandaoni, ili kuhakikisha kuwa unapata unachohitaji na pahali panapofaa pekee. Ili kuhimiza tovuti kutumia ulinzi huu wa ziada, tumefanya usimbaji fiche wa HTTPS kuwa moja ya ishara ambazo algoriti za Tafuta na Google hutumia wakati zinapoorodhesha tovuti katika matokeo yetu ya utafutaji.

Tunatoa zawadi za ulinzi ili kufichua hatari za kiusalama

Katika Google, tunaweka mipango ya zawadi za ulinzi ambayo huwalipa watafiti huru kutambua hatari za kiusalama katika huduma zetu na kuunda marekebisho ya usalama. Kila mwaka, tunatoa mamilioni ya dola katika ruzuku za utafiti na malipo ya kutambua hitilafu. Kwa sasa, tunatumia mipango ya zawadi za usalama katika bidhaa nyingi za Google, kama vile Chrome na Android.

Tunaruhusu zana zetu za usalama kutumiwa na wasanidi wa programu

Tunashiriki teknolojia yetu ya usalama tunapoamini kuwa itawanufaisha watumiaji. Kwa mfano, tunatoa Kichunguzi chetu cha Usalama cha Wingu la Google bila malipo kwa wasanidi programu ili waweze kukagua na kuchanganua programu zao za wavuti katika App Engine ili kutambua hatari za kiusalama.

Tunashiriki data ya shughuli zetu ili kuboresha usalama kwenye Intaneti

Tangu mwaka wa 2010 Google imechapisha Ripoti ya Uwazi, ambayo huangazia takwimu kwenye vitu kama vile viondoaji vya hakimiliki, maombi ya serikali kutumia data ya mtumiaji na mbinu za usalama kama vile Kuvinjari Salama. Pia, tunashiriki data kuhusu matumizi ya usimbaji fiche kwenye tovuti na barua pepe wavutini. Tunafanya hivyo ili kushiriki maendeleo yetu na wateja na pia kuhimiza watumiaji wengine kutumia viwango thabiti vya kiusalama ili kupata Intaneti salama kwa manufaa ya kila mtu.