Jinsi Matangazo Yanavyofanya Kazi

Hatuuzi maelezo yako ya kibinafsi.

Shughuli nyingi za biashara yetu zinahusu kuonyesha matangazo kwenye huduma za Google, tovuti na programu za vifaa vya mkononi za washirika wetu. Matangazo hutusaidia kuwapa watumiaji wetu huduma bila malipo. Tunatumia data kuonyesha matangazo haya lakini hatuuzi maelezo ya kibinafsi kama vile jina, anwani ya barua pepe na maelezo yako ya malipo.

Tunatumia data kukuonyesha matangazo yanayokufaa

Tunajaribu kukuonyesha matangazo yanayokufaa kwa kutumia data tuliyokusanya kutoka vifaa vyako, ikiwa ni pamoja na mambo uliyotafuta na mahali ulipo, tovuti na programu ulizotumia, matangazo na video ulizotazama na maelezo ya kibinafsi ambayo umetupa, kama vile umri, jinsia na mada unazopenda.

Kama umeingia katika akaunti, na kulingana na Mipangilio ya Matangazo uliyoweka, data hii hubainisha matangazo unayopata kwenye vifaa vyako vyote. Kwa hivyo, ukitembelea tovuti ya safari kwenye kompyuta yako kazini, huenda ukaona matangazo yanayohusu nauli za ndege za kuelekea Paris kwenye simu yako baadaye usiku huo.

Watangazaji wa bidhaa hulipia matangazo ambayo wateja huona au hufungua pekee.

Wakati watangazaji bidhaa wanapofanya nasi kampeni za matangazo, wanatulipa kulingana na utendaji wa matangazo hayo, wala si kulingana na maelezo yako ya kibinafsi. Hiyo inaweza kujumuisha kila wakati mtumiaji anapoangalia na kufungua tangazo, au anapochukua hatua baada ya kuona tangazo hilo, kama vile kupakua programu au kujaza fomu iliyopo.

Tunaonyesha watangazaji wa bidhaa matokeo ya kampeni zao

Tunawapa watangazaji data kuhusu utendaji wa matangazo yao bila kuwaonyesha maelezo ya kibinafsi. Katika kila hatua ya kukuonyesha matangazo, tunalinda maelezo yako ya kibinafsi na kuyaweka faraghani.

Jinsi matangazo yanavyotumika kwenye huduma za Google na tovuti za washirika

Tunatumia data kuonyesha matangazo yanayokufaa, iwe kwenye huduma za Google au tovuti na programu za vifaa vya mkononi za washirika wetu.

Baiskeli za rangi tofauti katika kidirisha cha kivinjari

Jinsi Matangazo ya Utafutaji yanavyofanya kazi

Unapotumia huduma ya Tafuta na Google, huenda matangazo yakaonekana karibu na matokeo husika ya utafutaji au juu yake. Mara nyingi, matangazo haya hutokana na utafutaji uliofanya na mahali ulipo. Kwa mfano, ukitafuta "baiskeli," unaweza kuona matangazo ya baiskeli zinazouzwa karibu nawe.

Katika hali nyingine, tunatumia data ya ziada kama vile utafutaji uliofanya awali au tovuti ambazo umetembelea ili kukuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi. Kwa kuwa tayari umetafuta "baiskeli," kama sasa utatafuta "likizo", huenda ukaona matangazo ya Utafutaji ya mahali unapoweza kuendesha baiskeli ukiwa kwenye likizo.

Matangazo ya Google katika Gmail yameangaziwa kwa rangi ya manjano

Jinsi matangazo ya YouTube yanavyofanya kazi

Unapotazama video kwenye YouTube, huenda ukaona matangazo yanayoendelea au kwenye ukurasa wa video. Matangazo haya yanatokana na video ulizotazama na data nyingine kama vile video ambazo umetafuta sasa au awali kwenye YouTube.

Kwa mfano, ukitafuta "vidokezo vya mitindo ya mavazi" au utazame video zinazohusu mapambo, huenda ukaona tangazo la vipindi vipya vya mfuatano vya mapambo. Matangazo haya husaidia kuwapa kipato watengenezaji wa video unazotazama.

Unaweza kuruka matangazo mengi ya YouTube kama hutaki kuyatazama.

Video ya YouTube ya mwanamke aliyefurahi ina tangazo ibukizi la miwani ya jua inayovuma

Jinsi matangazo ya Gmail yanavyofanya kazi

Matangazo unayoona katika Gmail yanatokana na data inayohusiana na Akaunti yako ya Google. Kwa mfano, shughuli zako kwenye huduma zingine za Google kama vile YouTube au Tafuta na Google zinaweza kuathiri aina ya matangazo ambayo unaona katika Gmail. Google haitumii maneno muhimu au barua pepe katika zilizo kikasha chako ili kukuonyesha matangazo. Hakuna mtu yeyote anayesoma barua pepe zako ili kukuonyesha matangazo.

Kivinjari chenye picha ya wasifu kina tangazo la mfuko maridadi wa kijani

Jinsi matangazo yanavyofanya kazi kwenye tovuti za washirika wa Google

Washirika wengi wa programu za vifaa vya mikononi na tovuti hufanya kazi nasi ili kuonyesha matangazo. Watangazaji hawa wa bidhaa huamua kuonyesha matangazo fulani kwa aina mbalimbali za watumiaji kulingana na maelezo ya kibinafsi ambayo wateja wetu wameshiriki nasi na data tunayokusanya kuhusu shughuli zako mtandaoni: kwa mfano, "wanaume walio na umri wa kati ya miaka 25-34 ambao wanapenda kusafiri."

Pia, tunaweza kukuonyesha matangazo kulingana na tovuti ambazo umetembelea awali. Kwa mfano, unaweza kuona tangazo kuhusu viatu vyekundu ambavyo uliongeza kwenye kikapu chako mtandaoni hapo awali lakini hukuvinunua. Tunafanya hivyo bila kufichua maelezo yoyote ya kibinafsi, kama vile jina, anwani ya barua pepe au maelezo ya malipo.

Dhibiti matumizi yako ya matangazo kutoka Google.

Tunakupa zana za kudhibiti aina za matangazo ambayo unaona ikiwa umeingia au hujaingia katika akaunti.

Kompyuta kibao yenye Mipangilio ya Matangazo na tangazo la miwani ya jua

Dhibiti matangazo kulingana na mambo unayopenda

Katika sehemu ya Mipangilio ya Matangazo, unaweza kudhibiti matangazo kulingana na mada unazopenda. Kwa mfano, ukitumia mipangilio ya Mapendeleo ya Matangazo, ili kuambia Google kuwa unapenda muziki wa Rumba, huenda ukaona matangazo ya rekodi zitakazotolewa hivi karibuni na tamasha zinazoandaliwa karibu nawe unapoingia katika akaunti ya YouTube.

Unapozima kipengele cha Mapendeleo ya Matangazo ikiwa umeingia katika akaunti, tataacha kukuonyesha matangazo yanayohusiana na mambo unayopenda kwenye huduma za Google na kwenye tovuti na programu za washirika wetu. Ikiwa umeondoka katika akaunti, kuzima Mapendeleo ya Matangazo kutaathiri huduma za Google mahali ambapo matangazo yanaonyeshwa pekee.

Tangazo la Google la gari la kijani lenye kitufe cha kukomesha tangazo juu yake

Ondoa matangazo ambayo huhitaji

Tunakupa uwezo wa Kukomesha Tangazo Hili kwenye aina nyingi za matangazo tunayoonyesha kupitia programu na tovuti za washirika wetu. Kwa kuchagua "X" katika kona ya tangazo, unaweza kuondoa matangazo ambayo hutaki kuona tena.

Kwa mfano, matangazo ya magari yalikuwa muhimu ulipokuwa unatafuta gari jipya, lakini baada ya kulinunua, inawezekana kuwa hutaki kuona matangazo zaidi ya gari ambalo tayari umenunua.

Kama umeingia katika akaunti na kulingana na Mipangilio ya Matangazo uliyoweka, udhibiti huu utatumika kwenye vifaa ulivyotumia kuingia katika tovuti na programu za washirika wetu.

Pia, unaweza kuzuia matangazo bila kuingia katika akaunti kwa kutumia kipengele cha Zuia Mtangazaji Huyu kwenye huduma za Google ambazo huonyesha matangazo.

Tangazo la miwani ya jua lenye kitufe cha maelezo sehemu ya juu kulia

Pata maelezo kuhusu data tunayotumia kukuonyesha matangazo

Tunataka kukusaidia uelewe vizuri data ambayo tunatumia kukuonyesha matangazo. Kipengele cha Kwa nini Unaonyeshwa Tangazo Hili hukuruhusu ubofye aikoni ili upate sababu ya kuonyeshwa tangazo mahususi. Kwa mfano, inawezekana unaona tangazo la fulana kwa sababu umekuwa ukitembelea tovuti za mitindo ya mavazi. Au, kama unaona tangazo la mkahawa, huenda ukagundua kuwa linatokana na mahali ulipo. Aina hii ya data hutusaidia kukuonyesha matangazo yanayohusu vitu vinavyoweza kukufaa. Kumbuka kuwa hatushiriki data hii na watangazaji wa bidhaa.